Malipo Kwa Tigo Pesa

[[{"type":"media","view_mode":"media_original","fid":"1233","attributes":{"alt":"","class":"media-image","height":"1458","typeof":"foaf:Image","width":"3958"}}]]

Malipo Kwa Tigo Pesa

Huduma hii inasaidia makampuni mbalimbali kupokea fedha kutoka kwa wateja wao wanaonunua bidhaa na kupata huduma mbalimbali. Huduma ni mahususi kwa makampuni yanayopokea kiwango kikubwa kwa malipo toka kwa wateja na pia hurahisisha malipo yao kwa wateja.Kuna faida lukuki kufanya malipo kwa Tigo pesa kutokana na urahisi wake katika kufanya malipo. Wateja wako wanaweza kulipia bili kutoka popote, wakati wowote muhimu ni kuwa na laini ya tigo iliyosajiliwa na ikiwa na pesa kwenye akaunti yake.

Kufungua Akaunti ya Tigo Pesa kwa kampuni yako tafadhali jaza  Fomu Ya Maombi  na utume kwa barua pepe kwenda TigoPesaCorporate@tigo.co.tz

Lipia Bili    

Wateja wetu sasa wanaweza kulipia bili kwa urahisi zaidi kwa kutumia huduma ya malipo ya Tigo Pesa .Kabla ya kufanya malipo yoyote ya bili hakikisha namba yako imesajiliwa Tigo Pesa na kuna kiwango cha kutosha katika akaunti yako. 

Jinsi ya kulipa bili yako

  1. Piga *150*01# kupata huduma za Tigo Pesa
  2. Chagua namba 4 kwa ajili ya ku "lipia bili"
  3. Chagua namba 3 kwa  “kupata majina ya kampuni”
  4. Chagua namba 1 kwa kuingiza "namba ya biashara" ya kampuni ambayo unataka kulipa  (Tafadhali rejea kiungo hapa chini kupata orodha)
  5. Ingiza "kumbukumbu nama" kwa kampuni husika
  6. Ingiza kiasi unachotaka kulipa
  7. Ingiza namba yako ya siri na thibitisha muamala wako