Tigo Pesa App

Tigo Pesa App

JINSI YA KUANZA KUTUMIA1.Programu hii inapatikana kwa simu zenye mfumo  wa  IOS na Android  au  kupitia  kiunganishi kinachopatikana katika  wavuti  yetu

2.Mara tu unapopakua programu hii  na kuanza kutumia unatakiwa kujisajili kifaa chako iwe ni simu ya mkononi au ipad .

3.Utatumia namba ya simu ya tigo ambayo imesajiliwa na Tigopesa na  namba yako ya siri ya Tigopesa

4.Kama kifaa chako hakitakupa  alama  ya uthibitisho  tafadhali nenda katika ujumbe wa mfupi wa maneno na ukopi na kupesti  pale palipoandikwa “ingiza alama ya uthibitisho uliyopokea”

5.Mara tu utakapojaza taarifa zako zote hakikisha unakubaliana na vigezo na masharti  kasha bofya kitufe cha OK kukamilisha usajili wako na utaanza kutumia programu  ya Tigopesa. MASWALI YA MARA KWA MARA

 1. Ni jinsi gani nitapakua programu ya Tigo Pesa?

Mteja anaweza kupakua programu kwa kufuata kiunganishi kipatikanacho katika wavuti ya Tigo Pesa au ujumbe mfupi uliotumwa kwake. Vilevile wateja wanaweza kutembelea hifadhi ya programu ya Apple na android na kuipekua moja kwa moja kutoka kwenye hifadhi hizo.

   

 1. Je ninaweza kupata wapi kiunganishi/ jinsi ya kupakua programu ya Tigo Pesa?

Kiunganishi kinapatikana kwenye wavuti ya Tigo Pesa au kwa kutembelea hifadhi ya programu moja kwa moja kwa kupitia simu yako.

 1. Je ni muda gani unatakiwa kupakua programu ya Tigo Pesa?                                                                                      

Programu ya Tigo Pesa itachukua muda kupakua kulingana na spidi ya intaneti .

 1. Je nitakatwa fedha zaidi nikitumia programu hii?                                    .                                                                  

Hapana. Utakatwa makato ya kawaida, na matumizi ya huduma ya data unapotumia huduma ya Tigo Pesa hayatakatwa.

 1. Je nitachajiwa kiasi chochote  ninapotumia programu hii?

Hamna makato yoyote ya kifedha atakayokatwa mteja kwa kupakua huduma ya programu ya Tigo Pesa.

 1. Je huduma zote zinapatikana kwenye programu ya Tigo Pesa?

Huduma zote zinazopatikana kwenye Tigo Pesa kupitia USSD, pia zitapatikana kwenye program za simu za kisasa.

 1. Je nitafanyaje endapo programu yangu itapata matatizo?

Hayo yakitokea: Angalia kama simu yako imeunganishwa na intaneti au wasiliana na huduma kwa wateja ya Tigo.

 1. Je ninahitaji nini ili niweze kutumia huduma hii?

Unachotakiwa ni: Simu yako yenye mfumo wa IOS au android yenye data/wifi na namba yako ya Tigo iliyosajiliwa.  

 1. Je naweza kutumia huduma hiyo kwenye mtandao mwingine?

Ndio, haijalishi ni mtandao upi wa simu unaotumia ilimradi tu wewe ni mtumiaji wa huduma ya Tigo Pesa iliyosajiliwa na unaweza kupokea alama ya uthibitisho ya ujumbe itakayotumwa kwa namba ya Tigo iliyosajiliwa.

 1. Je nitatumia namba ileile kwa kupata huduma Tigo Pesa?

Ndiyo, utatumia namba ya ileile ili kupata huduma ya Tigo Pesa unapofanya miamala kwa USSD *150*01#
11  Je itakuwaje nikipoteza simu yangu?

Unatakiwa kupiga simu huduma kwa wateja kuhakikisha simu yako inaondolewa usajili ,unaweza kupakua programu  ya Tigopesa katika simu nyingine na kuendelea kutumia

12  Pesa zangu zinaweza kuibiwa nikipoteza simu yangu?

Hapana pesa zako zitakuwa salama kwa kuwa akaunti yako inalindwa na namba yako ya siri ya Tigopesa

 1. Nitajuaje kama simu yangu inaweza kutumia programu ya tigopesa?

Unaweza kutembelea wavuti kuona aina ya simu zinazofaa na pia huongezwa kwa muda mara tu simu mpya inapoongezwa katika idadi

 1. Je itakuwaje nikisahau namba yangu ya siri?

Unaweza kurudisha namba yako ya siri kwa kupiga simu kituo cha huduma kwa wateja cha Tigo kwa namba 100 au tembelea maduka yetu ya  Tigo 1. Je programu hii inafamya kazi sehemu yoyote Tanzania?

Ndiyo,Programu inafanya kazi popote Tanzania ili mradi kifaa chako au simu imeunganisha na huduma za data,pia inaweza kufanya kazi dunia nzima ili mradi una huduma za data .

 1. Je kuna lugha gani katika programu?

Programu hii inapatikana kwa lugha mbili ya Kiswahili au kiengereza,mtumiaji ana uchaguzi muda wowote kubadili lugha anayotaka kutumia 1. Je ninaweza kuhifadhi kumbukumbu za  malipo yangu ya bili?

Ndiyo,unaweza kuhifadhi au kufuta muda wowote.Programu hii inakupa chaguo la kuhifadhi kumbukumbu ya malipo mara tu unapofanya miamala

 1. Je kuna usalama wa kiasi gani katika programu hii ?

Programu hii inatumia kifaa chako maalumu cha usalama kwako mteja,lakini tunakumbukusha wateja wetu kutotoa namba ya siri kwa mtu yoyote na pia hata wafanyakazi wa Tigo hawatakiwi kukuomba namba yako ya  siri.

 1. Je ninaweza kutumia namba yangu kwa huduma zote  kwa kupiga *150*01# na programu?

Ndiyo unaweza kutumia namba yako kwa huduma zote  kwa kupiga *150*01# au kwa kutumia programu ya Tigopesa 1. Ninaweza kupakua programu ya Tigopesa katika kifaa zaidi ya kimoja?

Ndiyo unaweza kupakua programu katika vifaa vingi kwa mara moja na kuweza kutumia katika vifaa vyote ulivyosajili na tigopesa ,unaweza kuona vifaa vyote vilivyosajiliwa na pia unaweza kuondoa usajili katika programu ya Tigopesa.PAKUA SASA

 [[{"type":"media","view_mode":"media_original","fid":"765","attributes":{"alt":"","class":"media-image","height":"80","style":"width: 110px; height: 80px;","typeof":"foaf:Image","width":"110"}}]][[{"type":"media","view_mode":"media_original","fid":"766","attributes":{"alt":"","class":"media-image","height":"80","style":"width: 110px; height: 80px;","typeof":"foaf:Image","width":"110"}}]]