Maswali ya Mara kwa Mara

Vertical Tabs

Sauti na Ujumbe Mfupi wa Maandishi

Sauti na Ujumbe Mfupi wa Maandishi

1 Mini kabang ina faida gani?

Faida ni

 • Dakika 20
 • Sms 100
 • Mb 8 
2 Ukomo wa mini kabang ni muda gani?


Masaa 24

Malipo ya Baada

Malipo ya Baada

1 Nani anaweza kujiunga na Postpaid?

Iko wazi kwa wateja wote wa Prepaid na wateja wapya wanaotaka kujiunga na huduma ya Postpaid.

2 Naunganishwa vipi kwnye Postpaid?

Unapaswa kutembelea moja ya maduka yetu ukiwa na mahitaji yote na tutakujazia fomu ya maombi tayari kwa kuanza.  Kuunganishwa kwa kampuni kutahitaji kamati ya kampuni husika kutembembelea duka la tigo mara zaidi ya moja.

3 Mkataba ni wa muda gani?

Mkataba ni kati ya miezi 18 na 24 ikitegemea mipango na mkataba unaweza kurejelewa.

4 Ni kwa muda gani akaunti yangu inaweza kuanza kufanya kazi?

Akaunti inaanza kufanya kazi punde tu vielelezo vyote vinavyohitajika vitakapokuwa vimewasilishwa na fomu ya maombi kuwa imejazwa.

5 Ni nani naweza kuwasiliana naye endapo nitakua na ulizo juu ya akaunti yangu?

Unapaswa kupiga namba 100; tunayo timu makini tayari  kukuhudumia. 

6 Ninapataje bili yangu ya mwezi?

Unapaswa kutoa anuani ya barua pepe wakati wa kujaza fomu ya maombi, kupitia anuani hiyo bili zako zitatumwa kila mwezi.

7 Nalipa wapi bili yangu?

Unaweza kutembelea duka letu lolote kwa malipo ya bili.

8 Naweza kulipa bili yangu kwa benki au Tigo Pesa?

Ndio, unaweza kulipa bili kupitia Tigo Pesa kwa kutumia namba ya Wakala 13263 kama umesajiliwa Tigo Pesa na Benki.

9 Naweza kulipia matumizi ya mbele?

Ndio unaweza kufanya malipo ya mbele ambayo yatahifadhiwa kwenye akaunti yako.

10 Je naweza kutumia namba yangu ya sasa kwenye Postpaid?

Ndio, namba ya sasa ya prepaid inaweza  kutumika kwenye Postpaid na pia unaweza kupata namba hyo hiyo kutoka kwa mtoa huduma tofauti ikiwa na kodi namba mpya ya  Tigo. 

11 Ni vigezo gani vinahitajika kujiunga na huduma ya Postpaid?

Watu binafsi

 • Nakala iliyoidhinishwa ya Kitambulisho cha Taifa, Passport au kitambulisho  kinachotambulika kinachofanana na hivyo vilivyotajwa
 • Nakala iliyoidhinishwa na serikali ya mtaa ya makazi yako au kibali maalum cha kazi kwa watu wasio raia.
 • Physical address – Anuani ya makazi
 • Barua kutoka kwa wadhamini wawili na vielelezo vya mawasiliano yao.
 • Maelezo ya Benki ya miezi mitatu iliyopita
 • Kiwango cha dhamana kutokana na kiwango cha dhamana
 • Saini mkataba kwa miezi 18 au 24 kulingana na mpango.

 

 Serikali, Shirika la Umma na Balozi.

 • Barua ya maombi ya huduma kutoka kwa mamlaka husika.
 • Kitambulisho kilichotolewa na Serikali/Ubalozi kwa mhusika
 • Anuani ya makazi (lazima ithibitishwe)
 • Kiwango cha dhamana kutokana na kiwango cha dhamana

Makampuni (Ushirika, Mashirika yasiyo ya kiserikali,Wafanyabiashara)

 • Nakala ya leseni ya biashara
 • Nakala ya Usajili wa VAT na TIN
 • Cheti cha ushirika.
 • letterhead ya kampuni na majina kamili pamoja na sahihi za wamiliki wa kampuninakala iliyoidhinishwa ya passport na idhini ya makazi ya wamiliki
 • Kiwango cha dhamana kutokana na kiwango cha dhamana
 • Anuani ya makazi (ni lazima ithibitishwe)
  • Maelezo ya benki kwa miezi 3 iliyopita
12 Naweza kubadilisha akaunti yangu kutoka Postpaid kwenda prepaid?

Ndio, unaweza kufanya mabadiliko na kinyume chake; ingawa mabadiliko yanazingatia vigezo na masharti ya Tigo.

Tigo Pesa

Tigo Pesa

1 Huduma hii ya Zoop inahusu nini ?

Huduma hii ya Zoop inatoa suluhisho la kuondoa urasimu katika malipom ya ada kwa baadhi ya shulle ikiambatana na kukusanya na kutunza kumbukumbu. Malipo yanafanywa  kwa kutumia TigoPesa.

2 Malipo ya Tanesco postpaid ni nini?

Huduma hii inawasaidia wateja wenye mita za zamani za Tanesco kuliopa bili kutumia Tigo Pesa

3 Nalipaje bili zangu kwa kutumia Tigo pesa?

Piga *150*01#

Chagua namba 4 “malipo”

Chagua namba 3 “kupata kumbukumbu namba “

Chagua namba 3 “chagua kampuni”

Kwenye orodha utapata chaguo la kulipa BILI 

4 Kwenye Malipo ya Zoop, Jinsi gani naweza kupata utambulisho wa malipo?

Utambulisho wa malipo hutolewa na shule husika ,inaweza kuwa ni namba ya usajili wa mwanafunzi au namba ya utambulisho kutokana na makubaliano ya Zoop na shule.

5 Kuhusu malipo ya Zoop, kampuni ya Zoop ni nini?

Zoop Tanzania company limited ni moja ya makampuni yaliyoingia makubaliano na taasisi za elimu Tanzania kurahisisha payment ya ada kutumia TIGOPESA.Zoop imesaidia shule nyingi ikiwamo Eagle BOYS secondary, Heritage English medium,.Mango school na kadhalika.

Internet

Internet

1 Kuhusu Facebook kwa USSD, Viwango vya gharama ni vipi?

1. Gharama ya kila siku Tsh. 99 tu.

2. Gharama za kila wiki 399 tu

2 Kuhusu Facebook kwa USSD, Najitoaje kwenye huduma?

Piga *148*01*4*02#

Chagua 00 kuendelea

Bonyeza *Marekebisho ya akaunti

Kisha 1 kujitoa

Rudi juu

3 Kuhusu Megaboksi, Nini cha ziada kwenye vifurushi hivyo?

I.  Kiwango bora cha data kwa bei nafuu

II. Kifurushi cha data cha Usiku ambacho kinampa nafasi mteja kutumia kati ya 11 usiku hadi 5 alfajiri kwa siku mbili.

III.  Mteja anaweza kujiunga muda wowote

IV.  Kinaweza kutumika kwenye simu yoyote yenye uwezo wa intaneti

V.   Vituo vyetu vya mauzo sasa vinaweza kuuza vifurushi vya data kwa malipo ya wazi kama inavyoonekana hapo juu

VI.  Angalia Salio kupitia *102*02#

4 Kuhusu Megaboksi, Najiungaje kwenye vifurushi vya Megaboksi?

Piga *148*00 #

CHAGUA NO 5 "VIFURUSHI VYA INTERNET"

KISHA chagua namba 1 chini "AINA YA KIFURUSHI" kwa kifurushi unachopenda.

5 Kuhusu 4G LTE, Je 4G LTE ni nini?

4G au LTE (Long Term Evolution) ni intaneti mpya yenye kasi na ubora wa kiwango cha juu.  Ukiwa na intaneti ya 4G utakuwa na uhakika zaidi wa kuwasiliana na kujiepusha na usumbufu wa kukata kwa intaneti. 

 

6 Kuhusu 4G LTE, Ni kipi cha ziada kwenye 4G ambacho hakipo kwenye 3G?

•        4G ina matumizi mengi zaidi ambayo yanaweza kutumika kwenye simu bila kigugumizi.

•         Uwezo wa kubadilishana mafaili na kupaitia vyombo vya habari mtandaoni kwa kasi na kwa wakati.

        . Uwezo wa kufikisha data zinazohitajika ndani ya muda mfupi.sactions.

7 Kuhusu 4G LTE, Naanzaje kutumia 4G?

Unapaswa kuwa kwenye eneo lenye 4G/LTE, laini ya 4G/LTE, kifaa kinachoweza kutumia 4G/LTE na kuwa na kifurushi cha 4G/LTE ili kufurahia huduma hii.