Tigo Pesa

[[{"type":"media","view_mode":"media_original","fid":"1009","attributes":{"alt":"","class":"media-image","height":"350","typeof":"foaf:Image","width":"950"}}]]

 Hii huduma inasaidia makampuni kupokea malipo kutoka kwa wateja wake au wanunuzi wa bidhaa na huduma. Huduma hii inawafaa makampuni yanayopokea malipo mengi kutoka kwa uma, yenye muonekano wa kikampuni na yanayotafuta urahisi na malipo ya muda muafaka kutoka kwa wateja wao. Hii inatoa manufaa mengi kwa kampuni yako kwa urahisi unaotoa kupokea malipo. Wateja wako wanaweza kulipa bili zao popote pale ili mradi uwe na laini ya tigo na salio kwenye tigo pesa yako.

Kufungua akaunti ya tigo pesa ya kampuni tuma email kwenda business@tigo.co.tz

Lipia Bili

Wateja wetu wa tigo pesa sasa wanaweza kulipa bili na huduma walizopokea kupitia huduma ya malipo ya tigo pesa .

Kabla ya kulipa bili yako hakikisha laini yako imesajiliwa na Tigo pesa na kuna salio la kutosha kwenye akaunti yako ya Tigo pesa

Jinsi ya kulipia Bili

1.   Kwa mteja alie sajiliwa piga *150*01# kupata huduma ya tigo pesa

2.   Chagua namba nne (4) kwa ” malipo”

3.   Chagua namba tatu (3) kwa malipo kwa kampuni”

4.   Chagua namba (1) kuweka namba ya biashara kwa kampuni unayotaka kulipia

5.   Ingiza namba ya kumbukumbu ya iyo kampuni

6.   Ingiza kiasi cha malipo

7.   Ingiza namba yako ya siri kuhakikisha.