Reach for change 2014

SHIRIKISHA WAZO LA KIBUNIFU, FADHILIWA NA ULETE TOFAUTI

 

Je, wewe ni mjasiriamali wa kijamii unayefanya kazi ya kuboresha maisha ya watoto na jamii kwa ujumla? Na unatumia vifaa vya tehama kukuza maendeleo yako? Una wazo la kibunifu la kuleta omabadiliko duniani na pia shauku ya kuleta mabadiliko hayo? Shirikisha wazo lako tutekeleze pamoja !

 

Tigo Digital changemakers competition (Shindano la Tigo Waletamabadiliko wa kidigitali) itatoa zawadi ya kiasi cha dola elfu 20 za marekani kwa washindi kusaidia mradi pia utasaidiwa kupewa mafunzo ya kuboresha wazo lako toka kwa wafanyakazi wa Tigo na washirika wetu Reach for change kuboresha wazo kikamilifu.Wajasiriamali ambao mawazo yao hayana matumizi ya teknolojia katika utendaji wao pia wanaweza kushiriki ili mradi wazo hilo lina uwezekano wa kutumia teknolojia ya digitali kuleta ufanisi zaidi.

Matumizi ya teknolojia ya digitali yanaweza kuonekana katika  namna zifuatazo;

 

  • Kutumia simu,intaneti,na teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA), kama namna moja ya kuchangia suluhu
  • Uwezo na kutumia mtandao kwa simu za mkononi, pia TEHAMA kuboresha hali ya maisha na maendeleo ya jamii
  • Kupeleka na kukuza upatikanaji wa mawasiliano kwa jamii zilizosahaulika

 

Pata ufadhili kwa taasisi yako na mafunzo na usimamizi makini na utambuzi wako wa matatizo ya watoto na jamii kwa ujumla huku ukisaidiwa na washauri toka Tigo na wataalamu wa kimataifa

 

Ibuka kuwa kinara,ibuka kuwa Digital change maker (Mleta mabadiliko wa kidigitali)

JIUNGE SASA!