Reach for change 2012

Tigo Reach for Change ni mpango unaosaidia wajasiriamali wa kijamiii barani Afrika ambao wana shauku ya kukuza haki za watoto,wazo la kibunifu litakalobadilisha maisha ya watoto na kuweka usawa huku ukiwa na ari ya kuboresha .Wajasiriamali watapata ufadhili na mafunzo katika mfumo maalumu wa mafunzo washauri wa Tigo na wataalamu kusaidia kuboresha wazo lako.

Safari ya kuchagua wajasiriamali mashuhuri wa kijamii nchini Tanzania ilianza Septemba 2012 ambapo watu wapatao 3000 walionyesha kuvutiwa na mpango huu na 1000 waliwasilisha maombi. Kwa msaada kutoka kwa wafanyakazi wa Tigo maombi yote yalichujwa kwa kutumia vigezo mahsusi vya mjasiriamali wa kijamii na wazo likawasilishwa. Mchakato wa kuchuja ulikuwa wa kina na uwazi mkubwa kuhakikikisha tunapata wazo bora kutoka kwa mtu sahihi mwenye dhamira ya kuboresha maisha ya watoto. Kwa sababu hii wataalamu wa Kitanzania katika nyanja ya Haki za Watoto walishirikishwa wakati wa kupitia Mpango wa Biashara wa Mjasiriamali wa Kijamii kupata 15 ambao walihojiwa na safu ya Tigo na Reach for Change.

Disemba 2012, timu ya Tigo na Reach for Change kwa furaha kubwa  iliwatangaza wajasiriamali wakubwa wa 3 wa kijamii ambao wataungana na mtandao wa vingozi wengine wa mabadiliko wa Africa ambapo Tigo inafanya kazi. Wajasiriamali hao ni hawa wafuatao:

Brenda Deborah Shuma - Wezesha watoto wenye ulemavu kwa mafunzo ya vitendo.

Watoto wenye ulemavu wapo kwenye moja ya makundi yasiyokubalika zaidi nchini Tanzania. Mara nyingi huwa wanabaguliwa na jamii na watoto wengine, wananyimwa haki ya kupata elimu, na wanakoseshwa nafasi ya kujiandalia malengo yenye mafanikio katika maisha yao mbele. Brenda Deborah Shuma anapambana na tatizo hili kwa kuwawezesha watoto wenye ulemavu kupata mafunzo kwa vitendo wanayohitaji kujipatia kipato na kuandaa maisha yao ya mbeleni.

 

Nyabange Chirimi - Madarasa yanayotembea kwa ajili ya Watoto wa Mtaani

Idadi ya watoto wa mtaani nchini Tanzania ni kubwa na inaongezeka. Wanaishi mitaani bila kuwa na jinsi ya kupata mahitaji muhimu kama chakula, malazi na elimu.

Nyabange Chirimi anapambana kuwaleta watoto wa mtaani katika mfumo sahihi wa elimu kuheshimu haki ya kupata elimu na malengo yao. Nyabange anafanya hili kwa kutoa elimu mahali walipo watoto na katika muundo ambao italandana na matakwa yao maalumu na mahitaji. Hivyo watoto wanapata msaada  na kupimwa ili waweze kuingia kwenye mfumo sahihi wa elimu.

 

Thadei Msumanje - Kuboresha mafunzo kupitia ICT

Watoto wengi wanaoishi vijijini hawapati fursa ya ICT na hii inaongeza pengo la kidigitali nchini kati ya kijijini na mjini. Thadei Msumanje anataka kutatua tatizo hili kwa kuleta ICT kwa watoto wanaoishi katika jamii za vijijini. Msumanje ataambatanisha mafunzo ya ICT na mfumo wa elimu kama elimu ya awali kuhakikisha manufaa ya ICT katika mfumo wa elimu yanapatikana kwa watoto wa Tanzania wakiwemo watoto wanaoishi vijijini.

 

Kwa miradi hiyo hapo juu, ni wazi kwamba watu wengi watanufaika ingawa vitendea kazi sahihi na usaidizi unahitajika kwa hali na mali. Vyote hivyo vinaletwa na mpango maalumu ambapo Change Leaders (Viongozi wa Mabadiliko) watapokea usaidizi wa kibiashara ili kuendeleza, kupima na kuwezesha mikakati yao kwa kipindi cha mpaka miaka mitatu. Baada ya kuweka mikakati Viongozi wa Mabadiliko watapewa washauri 2-3 na wataalamu kutoka Tigo kuwasaidia kuendeleza na kupima miradi yao.