Kusajili wa Kuzaliwa kwa Njia ya Simu

Tigo Tanzania kwa kushirikiana na RITA  ( Wakala wa usajili wa vizazi na vifo) pamoja na UNICEF wanaungana kutengeneza mfumo  mpya wa usajili vizazi na kusaidia watoto wenye umri chini ya miaka mitano kuwa na na vyeti vya kuzaliwa .Mfumo mpya wa usajili utatumia njia za kibunifu kwa kutumia programu ya  simu ambayo itakayoletwa na Tigo.

Kifaa cha simu kitarahisisha taratibu za usajili wa mtoto kwa kuingiza taarifa za usajili katika simu ya mkononi ambayo itatuma data katika mfumo wa kati wa database wa RITA katika muda mfupi .Programu hii imetengenezwa na kuweza kufanya kazi katika kila aina ya simu zenye mifumo tofauti.

Jinsi gani inavyofanya kazi

Taarifa za usajili wa motto huingizwa katika simu na wakunga au viongozi wa vijiji au kata  na hutumwa kwa kutumia ujumbe mfupi wa maneno na kupokelewa katika kituo kikuu cha taarifa cha RITA . Kinachotakiwa ni kuwa na simu na laini ya Tigo.

Kulingana na Takwimu za afya za Tanzania zilizoendeshwa mwaka 2010,asilimia 16 tu ya watoto walio na chini ya miaka mitano wamesajiliwa na mamlaka za kiserikali , na kati ya hao asilimia 6 wamepata vyeti vya kuzaliwa .Hivyo basi kinachotakiwa ni kuweza kutatatua changamoto hii ni kusaidia kuandikisha usajili wa vizazi kwa watoto na kuweza kuimarisha usajili wa vizazi na usajili kwa mamlaka husika.Malengo yetu ni kusajili watoto laki 9 walio na umri chini ya miaka mitano katika kipindi cha miaka miwili.Mkakati huu utaendeshwa kwa awamu tukianza na mbeya kama awamu ya kwanza tukifuatia mikoa ya Mwanza,Geita, Shinyanga, na Simiyu.

Ubunifu huu umekuja katika muda mwafaka ambapo kuna maendeleo makubwa afrika yaliyoletwa na matumizi ya simu za mikononi.Kupitia juhudi hizi zinazoletwa na Tigo katika kujihusisha na jamii kuweza kuwasaidia kuleta maendeleo kupitia mfumo wa kidigitali.Hivyo basi tunajivunia kuwa kampuni ya kwanza kushirikiana na Rita na UNICEF kuhakikisha kila motto anapata cheti cha kuzaliwa.

Kujua zaidi kuhusu mkakati wa USAJILI WA VYETI VYA KUZALIWA bofya hapa.