Wezesha Wanawake kwa Maendeleo

Wezesha Wanawake kwa Maendeleo ni mkakati unaoratibiwa na Tigo pesa katika kuleta usawa wa kijinsia katika biashara za huduma za Kifedha  kupitia simu za mikononi wakati huo wakitoa mikopo rahisi kwa mawakala wanawake  wapatao 3200 na mafunzo kuweza kuboresha biashara zao.Mkakati huu umetekelezwa kwa kipindi cha miezi 18 kwa ushirikiano na taasisi ya Cherie Blair Foundation for Women ( CBFW) ,Usaid na FINCA , na ilizinduliwa mwaka 2013 na Mama Cherie Blair .

Imethibitika kuwa kuna ombwe kubwa ya kijinsia  katika biashara za huduma za kifedha  kupitia simu za mikononi licha ya kuwa kuna fursa kubwa kutokana na kukua kwa kasi kwa sekta ya simu za mikononi hususani katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania. Hivyo basi kupitia mkakati huu utatengeneza fursa nzuri kwa mawakala wanawake kwa kuwahakikishia masoko ya huduma za kifedha na mafunzo ya bure kuweza kuboresha biashara zao. Wanawake watakaoshiriki katika mpango huu watapata nafasi ya kuweza kupata mikopo katika taasisi iliyojiimarisha katika kutoa mikopo ijulikanayo kama FINCA na mafunzo ya bure kuweza kuboresha biashara zao.

Kuwezeshwa  kifedha na mafunzo ya biashara yana lengo kuwasaidia wanawake kuanza biashara kama mawakala wa huduma za kifedha kupitia simu au kwa mawakala waliopo kuweza kuboresha biashara zao. Kwa kuongeza ushiriki wa wanawake katika bishara ya huduma za kifedha kwa kupitia simu za mkononi tunategemea kuona wanawake wengi wanaanza kutumia huduma hizi kwa mahitaji binafsi au kwa kibiashara .Mategemeo yetu mengine ni kuongeza mtandao mpana , uthubutu na kuongeza kipato chao.

Kujua zaidi kuhusu WEZESHA WANAWAKE KWA MAENDELEO bofya hapa na hapa.